GULAMALI AANDIKA HISTORIA ILONGERO: MKATABA WA UJENZI DARAJA LA MGORI WASAINIWA
Mbunge wa Jimbo la Ilongero, Haiderali Hussin Gulamali, ameandika historia leo tarehe 3/03/2026 baada ya kushuhudiwa rasmi utiaji wa saini wa mkataba wa ujenzi wa Daraja la Mgori – mradi utakaotekelezwa ndani ya miezi 8 kuanzia sasa. Hatua hiyo imekuja ndani ya siku 100 tangu kuapishwa kwake, ikiwa ni matokeo ya juhudi zake za haraka na za kimkakati. Ndani ya siku 30 tu baada ya kuwa mbunge, aliwaongoza baadhi ya madiwani kwenda kuonana na Waziri wa TAMISEMI, Riziki Shemdoe, kuwasilisha changamoto zinazowakabili wananchi wa Ilongero, ikiwemo tatizo sugu la korongo la Mgori. Kwa muda mrefu, korongo hilo limekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, huku likihatarisha maisha ya wananchi wakati wa mvua kwa kusombwa na maj...